The House of Favourite Newspapers

PSG Nyumbani Kuwavaa City Leo

0

MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inaendelea tena leo ambapo matajiri Manchester City wanatarajiwa kuvaana na PSG.

Huu ni mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali wa timu hizo ambao unatajwa kuwa utakuwa mkali na wa kuvutia.

 

Kocha wa Man City, Pep Guardiola, ambaye amekuwa akifanya vizuri kwenye Ligi Kuu England kwa kipindi cha miaka mitano alichokaa hapo anapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza akiwa na Man City.

 

Katika mchezo huo ambao PSG watakuwa nyumbani kwao kwenye Dimba la Parc des Princes, Guardiola alisema juzi kuwa timu yake ipo tayari kwa ajili ya mechi hiyo na hawana hofu yoyote.“Tupo tayari kwa kuwa tupo nusu fainali, hii ni hatua kubwa kwa timu yetu na hakika kila mmoja anafahamu hilo.

 

“Tunafahamu kuwa PSG ni timu kubwa yenye wachezaji wengi mahiri, hakika hata sisi tupo imara ndiyo maana tupo hapa leo, naamini kuwa tunaweza kufanya vizuri kwenye mchezo huu,” alisema Guardiola. Kwa upande wa PSG, kocha wao Mauricio Pachettino alisema kuwa wachezaji wake wote wapo fiti na hakuna hofu kuwa Kylian Mbappe ataukosa mchezo huo.

 

“Awali ilikuwa ikielezwa kuwa Mbappe ataukosa mchezo huu, hapana, kwangu na madaktari wa timu tunafahamu kuwa yupo tayari kwenye mchezo huu.“Nafikiri hii ni mara ya pili timu hii inakwenda fainali na tumekuwa tukitamani kwa nguvu kubwa kuchukua ubingwa huu, nafikiri tunaweza kufanya vizuri hapa kwetu na ugenini,” alisema Pachettino.

Leave A Reply