The House of Favourite Newspapers

PUMZIKA KWA AMANI IKUPA NGAO

Tunasikitika kutangaza kifo cha mwanafunzi mwenzetu wa Chuo Kikuu cha Tumaini wa Shahada ya Kwanza ya Mawasiliano ya Umma ( BA- in Mass Communication), Ikupa Ngao aliyefariki leo Desemba 20, 2018 katika Hospitali ya Mloganzila baada ya kuugua ghafla.

 

Ikupa Ngao aliumwa kichwa ghafla Septemba 7 mwaka huu na Septemba 8 alizidiwa na kuchukua pikipiki ili imuwahishe hospitali lakini aliishiwa nguvu akaanguka wakati anapelekwa hospitali,  alipoteza fahamu na hakurudiwa na fahamu tena.

 

Sisi wanafunzi wenzake tumesikitishwa sana na kifo cha mwenzetu Ikupa Ngao na tunamkumbukwa kwa jinsi tulivyokuwa tunashirikiana kimasomo darasani na hata nje ya darasa.

 

Tunawaomba wote ambao mtasoma tanzia hii muungane nasi kumuombea Ikupa Ngao ili mwenyezi Mungu roho yake ailaze mahali pema peponi – Amina.

 

Ni sisi wanafunzi wenzake wa mwaka wa pili wa Shahada ya Mawasiliano ya Umma. 

Chuo Kikuu cha Tumaini, Dar.

Comments are closed.