The House of Favourite Newspapers

Q-Chief Aweka Bayana Bifu Lake na Director Hanscana, Bofya Hapa!

q-chief-1 Na Mwandishi wetu

NGULI wa Bongo Fleva, Q-Chief, ameweka bayana kuhusu kuwepo na bifu kati yake na mwandaaji wa vodeo za muziki hapa nchini, Director Hanscana ambapo ameeleza kuwa mashabiki wa kwenye mitandao ya kijamii hupenda kuyakuza mambo na kuyachukulia ndivyo sivyo.

Q-Chief ameyabainisha hayo wakati akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wetu kuhusu bifu hilo, wakati akifanya Exclusive Interview na Global TV, jana Ijumaa, Desemba 2.

q-chief-2

Alijibu: “Hanscan is a human like another human, don’t mind what is minding, is like another human.

“Mimi niliulizwa swali kuhusu directors wa video wa hapa nchini kama tunaweza kufanya nao kazi au vipi, nikasema maoni yangu, kwa sasa sijajiandaa kufanya kazi na director wa Tanzania, sio kama hawawezi kufanya kazi, ni watendaji wazuri wa kazi lakini najaribu kuangalia location zangu kwa Tanzania. Most of them zimetumika unakwenda kushuti unaambiwa Twenty Percent alikuja kushuti hapa na Hanscana jana.

HanscanaHanscana.

“Kwa hiyo kuingiza jina la Hanscana kwenye huo mfano, moja kwa moja ikawa kama bifu kwamba mimi nimemzungumzia Hanscana?”

“I have seen the best directors hapa na sijawahi kufanya nao bifu, kama Adam Juma, my brothers nawaheshimu sana kwenye game, akina Nick Dizzo…..”

“Why Hanscana?…….

“Ninaheshimu kazi zake, napenda kazi zake ni sehemu ya juhudi zake…..

“For the time being sikuona umhimu wa kurekodia hapa, ndiyo maana nikatoka nje ya nchi.” Alisema Q-Chief na kumsihi Hanscana aendelee kukaza buti na kufanya kazi kwa bidii zaidi.

Akizungumza kwenye mahojiano hayo, Q-Chief alizungumzia pia ujio wa ngoma yake mpya ambayo amemshirikisha mwanamziki kutoka nchini Nigeria, Patoranking na kueleza kuwa wimbo huo tayari umekamilika, hivyo siku yeyote atauachia rasmi.

halotel-strip-1-1

Comments are closed.