The House of Favourite Newspapers

Queen Darleen na Mke Mwenza Gari Limewaka

0

MSANII wa Bongo Fleva ambaye kwa sasa ni mke wa pili wa Isihaka Mtoro, mwanadada ‘Queen Darleen’ ameanza kuvaana na mke mwenziye anayefahamika kwa jina la Sabra kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

 

Hayo yamejiri baada ya wawili hao; Queen Darleen na Sabra kuanza kutupiana madongo kwenye mitandao ya kijamii, huku kila mmoja akitamba kupendwa.

 

Mke mdogo ambaye ni Queen Darleen, alianza kwa kutuma video fupi iliyoonekana akikumbatia picha ya mume wao Isihaka, jambo lililoleta wivu na kupelekea mke mkubwa (Sabra) kuingia hewani (live) na kumrekodi kwa mbali mume wao Isihaka akiwa kitandani huku akiwa tumbo wazi.

Baada ya muda kidogo, Queen Darleen aliandika ujumbe mfupi wa kejeli akimjibu mke mkubwa akisema “Naskia kuna mtu kaingia Insta live kwake, lakini anashut kama jambazi kaingia nyumbani na kuiba Sh milioni 10 na mjegejoo, baba ovyooo.

 

”Hatua hiyo, ilisababisha Sabra kujibu na kuandika ujumbe, “Hivi na nyie mnapendwa kama mimi…? huba linanizidia natamani kutoa ushuhuda mwenzenu… napendwa alafu napendwa tena,” alisema Sabra.

 

Majibizano haya ya mitandaoni ya wake wenza hao ambayo yameonekana kuwa sawa na kutupa jiwe gizani, yamezua sintofahamu kwa mashabiki zao.Mmoja wa mashabiki waliandika katika ukurasa huo kumponda Queen Darleen na kumuonya kuwa aache kidomodomo.

🔴#LIVE: POLISI WATOA KAULI MLINZI WA MEMBE KUKAMATWA | MAGUFULI, LISSU BODA KWA BODA KUSAKA KURA

Leave A Reply