The House of Favourite Newspapers

Rai Yatolewa Kwa Wananchi Kulinda Na Kutunza Amani Ya Muungano – Video

0
Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Dkt Suleiman Jafo.

Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Dkt Suleiman Jafo ametoa Rai kwa Wananchi wote kuulinda na kuutunza muungano kwa gharama yoyote ile kwani ni wa kipekee Afrika na Duniani kwa ujumla.

Wazi Jafo ametoa Rai hiyo katika mkutano wake ma wandishi wa habari ikiwa ni kuelekea miaka 60 ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar ulifanyika Jijini Dodoma Leo wakati akielezea mafaniko ya muungano huo.

“Natoa rai kwa Wananchi wote wa Tanzania kuendelea kuuenzi, kukulinda na kuutunza Muungano wetu adhimu, ambao umedumu kwa miaka 60. Huu ni muungano wa kipekee barani Afrika na duniani kwa ujumla”.

Sambamba na hayo pia Waziri amezungumzia mafanikio katika nyanja mbalimbali ikiwemo mafanikio ya kiuchumi,kijamii na Mazingira ambapo huku kote kumekuwa na mafanikio makubwa sana.

“Ndugu Wanahabari;Tangu kuasisiwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais inatekeleza na kuratibu shughuli ya hifadhi na usimamizi wa Mazingira ili kuhakikisha matumizi sahihi ya rasilimali asili na maendeleo endelevu kwaajili ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho”.

Idara ya Mazingira ilianzishwa mwaka 1992 ikiwa ni juhudi za Serikali kuhimiza uhifadhi na usimamizi wa Mazingira nchini kama ilivyohimizwa na Azimio la Rio mwaka 1992 linalozitaka nchi zote duniani kutambua uhusiano uliopo kati ya maendeleo na mazingira.

Kufuatia kuanzishwa kwa Idara ya Mazingira, Tanzania iliridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa inayohusu Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira, ambapo katika kutekeleza Azimio Rio la Mwaka 1992, Tanzania iliandaa Mpango wa Kwanza wa Taifa wa Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (National Environmental Action Plan – (NEAP) mwaka 1994.

Maadhimisho hayo ya Muungano hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 26 mwezi wa 4.

Leave A Reply