The House of Favourite Newspapers

Rais Aapishwa Ghana Baada ya Ghasia Bungeni

0

NANA Akufo-Addo ameapishwa kuwa rais wa Ghana kwa muhula wa pili, siku moja baada ya ghasia kutokea bungeni. Askari waliagizwa kufanya tukio ambalo si la kawaida katika taifa ambalo limekuwa na demokrasia imara zaidi Afrika.

 

Addo alimshinda mpinzani wake, rais wa zamani wa nchi hiyo, John Mahama, mwezi Desemba katika uchaguzi uliokuwa una ushindani mkali. Anakabiliwa na changamoto kubwa mbili, moja ikiwa ni kukabiliana na janga la virusi vya corona na suala la kuinua uchumi.

 

Ghana ina visa zaidi ya 50,000 vya virusi vya corona na kama mataifa mengine, inakabiliwa na changamoto ya uchumi kushuka. Mambo yamebadilika Jumatano baada ya kura za kumchagua spika mpya.

 

Ghasia ziibuka bungeni baada ya mbunge mmoja kujaribu kunyakua boksi la kura na kukimbia nalo nje ya jengo la bunge.

 

“Kulikuwa na uvunjifu wa sheria na utaratibu,” alisema mbunge aliyeteuliwa, Kwame Twumasi Ampofo, kutoka chama cha upinzani cha National Democratic Congress (NDC).

 

Mgogoro kati ya wabunge wa NDC na wa Akufo-Addo wa chama cha New Patriotic Party (NPP), uliibuka baada ya walivamiwa na askari ambao waliingilia kati ghasia hizo.

 

Mwanachama wa NDC, Mbunge, Alban Bagbin, aliapishwa baadaye kuwa spika. Hii ni mara ya kwanza kuwa na spika kutoka chama tofauti na rais.

 

Mapema wiki hii, rais Akufo-Addo aliwataka wabunge waungane na  kufanya kazi kwa pamoja. Vyama hivyo viwili vilikuwa na wabunge idadi sawasawa.

Leave A Reply