The House of Favourite Newspapers

Rais Afunguka Watu Walivyokufa Ubungo – Video

0

 

RAIS John Magufuli amesema kabla ya ujenzi wa daraja la juu la Ubungo ‘Kijazi Interchange’ eneo hilo lilikuwa chanzo cha ajali na vifo vya wagonjwa waliokuwa wakiwahishwa hospitali.

 

 

Akizungumza leo Jumatano Februari 24, 2021 katika uzinduzi wa daraja la juu la Ubungo, kiongozi mkuu huyo wa nchi amesema katika kumbukumbu yake, wapo walipoteza maisha katika barabara hiyo na wakati wa kampeni sajenti mmoja aliyekuwa akiendesha pikipiki alifariki.

 

 

“Eneo la Ubungo lilikuwa na shida. Ninajua wapo watu walipoteza maisha yao hapa kwa kuchelewa hospitali, safari za uwanja wa ndege wakachelewa ndege, wengine walipoteza wachumba kwa kupoteza kufunga ndoa na wapo walioachika ambao walichelewa kufika nyumbani kwa sababu ya matatizo ya hapa Ubungo, ni mahali ambapo palileta shida jijini Dar es Salaam, leo ni siku ya furaha kwa kila mwana Dar es Salaam,” amesema Rais Magufuli.

 

 

Amesema mwaka 2017 alifika eneo hilo akiwa na rais wa benki ya dunia, “siku hiyohiyo nilimuomba aje kuweka jiwe la msingi, tulifanya hivyo kwa kuwa tulikuwa tunahitaji pesa tungeweza kulijenga wenyewe, lakini na sisi matajiri wa Tanzania tuliamua kwenda kukopa benki ya dunia.”

 

 

Hata hivyo Rais aliahidi kujenga madaraja mengine 10 jijini humo ili kupunguza msongamano wa magari na ajali.

 

 

Leave A Reply