The House of Favourite Newspapers

Rais Ataja Siri Nzito ya Ronaldo na Zidane

0
Cristiano Ronaldo na Zinedine Zidane.

RAIS wa Real Madrid Florentino Perez, amewataja Cristiano Ronaldo na Zinedine Zidane kuwa ndiyo nembo ya klabu hiyo kutokana na mafanikio yao ndani ya timu hiyo.

Perez ameeleza kuwa Real Madrid inajivunia uwepo wa watu hao muhimu ndani ya klabu yao Cristiano Ronaldo kama mchezaji aliyesaidia kupataikana kwa mafanikio mengi pamoja na Kocha Zinedine Zidane ambaye ameiongoza Madrid kupata mafanikio ndani ya misimu miwili.

“Tunatakiwa kujivunia nyota wetu hawa Ronaldo na Zidane kwasababu wameipa klabu mafanikio makubwa, Ronaldo ni mchezaji bora duniani na Zidane ni kocha bora duniani tuna kila sababu ya kuwaita nembo ya klabu”, amesema Perez.

Ronaldo mwenye miaka 32 ameiwezesha Real Madrid kushinda mataji 13 tangu jiunge na timu hiyo mwaka 2009 akitokea Manchester United.

Zidane akiwa na miaka 45 ameiwezesha Madrid kuwa klabu ya kwanza kutetea ubingwa wa UEFA pamoja na kurejesha makali ya kutwaa La Liga mbele ya mahasimu wao Barcelona.

Leave A Reply