The House of Favourite Newspapers

Rais Colombia Ashinda Tuzo Ya Nobel Ya Amani

El presidente Juan Manuel Santos ratificó el apoyo del gobierno Nacional a los programas dirigidos al sector cafetero durante el Acuerdo por la Prosperidad número 66 en Pitalito, Huila (Colprensa – Cortesía Presidencia).Rais Juan Manuel Santos.

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos leo ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Nobel ya amani kwa mwaka 2016. Rais huyo anaingia kwenye orodha ya viongozi wengine duniani waliowahi kushinda tuzo hiyo.

Mpaka sasa viongozi 25 wa juu wa serikali duniani kote wamewahi kushinda tuzo na 14 kati yao walikuwa madarakani.

Sababu kubwa ya Rais Juan kushinda tuzo hiyo ni juhudi za rais huyo kutaka kumaliza mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 50 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 220,000 huku wengine zaidi ya milioni sita wakikimbia makazi yao.

Tuzo hiyo ilianza kutolewa tangu mwaka 1901- hadi sasa.

juan-4…Akisisitiza jambo.juan-2Wakibadilishana mkataba wa amani na kundi la FARC.

juan-3Rais wa Cuba akiwashika mikono kama ishara ya kuwapatanisha.

Wengi wanajiuliza inakuwaje Rais huyo apate tuzo ili hali kashindwa kusimamia hata suala la upatanishi ndani ya nchi yake mwenyewe? Kwasababu mazungumzo ya amani kati ya serikali yake na kundi la waasi la FARC yamevunjika.

Na Leonard Msigwa/GPL.

 

 

Comments are closed.