The House of Favourite Newspapers

Rais Joe Biden Amteua Karine Jean-Pierre kuwa Msemaji wa Ikulu ya White House

0
Karine Jean-Pierre

Rais wa Marekani Joe Biden amemteua Karine Jean-Pierre kuwa Msemaji wa Ikulu ya White House na kumfanya kuwa mtu wa kwanza mweusi kushika cheo hicho cha hadhi ya juu katika Ikulu ya Nchi hiyo.

 

Katika taarifa yake Rais Biden amesifu uzoefu, talanta na uadilifu wa Jean-Pierre akisema kwamba anajivunia kutangaza kuteuliwa kwake kama Katibu wa habari wa Ikulu huku Msemaji wa sasa wa Ikulu hiyo Jen Psaki akiandika kwenye Twitter kwamba Jean-Pierre atakuwa Mwanamke wa kwanza mweusi kufanya kazi kama Katibu wa habari wa Ikulu ya White House.

 

Jean-Pierre mwenye umri wa miaka 44 aliwahi kufanya kazi kwenye kampeni za Rais mstaafu Barack Obama mwaka 2008 na 2012 na pia kwenye kampeni ya Joe Biden mwaka 2020 kabla ya kujiunga na timu ya Rais huyo ndani ya Ikulu.

Leave A Reply