The House of Favourite Newspapers

LIVE: Rais Kenyatta Azindua Treni Ya Kisasa Mombasa

0

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, leo amezindua treni ya kwanza ya kusafirisha mizigo na abiria katika reli mpya ya kisasa iliyojengwa kutoka Mombasa hadi Nairobi.
Reli hiyo ni ya urefu wa kilomita 472 na treni zitakuwa zikisafiri kwa kasi ya wastani ya kilomita 120 kwa saa.
Treni hiyo itachukua muda wa saa nne  na nusu kufika Nairobi, safari ambayo huchukua karibu saa nane kwa kutumia basi.

Ujenzi wa reli hiyo ya kisasa inayojulikana kama Madaraka Express, umegharimu KSh. Bilioni 40 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 800 za Tanzania.

 

Treni hiyo baada ya kuzinduliwa, iliondoka Mombasa saa 5:11 asubuhi hii kwa hiyo inatajiwa kufika jijini Nairobi saa 9:11 alasiri.

Leave A Reply