The House of Favourite Newspapers

Rais Kikwete azindua mradi wa kusaga kokoto Pongwe Msungura

0

1

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuzindua mradi wa kusaga kokoto uliopo katika kijiji cha Pongwe Msungura Wilayani Bagamoyo jana. Kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt.Hussein Mwinyi, Wa pili kulia, ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael Muhuga,wapili kushoto ni Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Yasemin Eralp, watatu kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ANIT ASFALT Bwana Semih Yaran, na wanne kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.

3Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi wa Pongwe Msungura wakati wa ufunguzi wa mradi wa kusaga kokoto jana.

2

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt.Hussein Mwinyi na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhuga wakati wa uzinduzi wa mradi wa kusaga kokoto. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.

4

Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Mhe. Yasemin Eralp akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mradi wa kusaga kokoto jana.

5

Kikundi cha sanaa cha JKT kikitumbuiza wageni wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa kusaga kokoto.

6

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili katika kijiji cha Pongwe Msungura kuzindua mradi wa kusaga kokoto. Aliyesimama pembeni ya Rais ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael Muhuga. Mradi huu unaendeshwa kwa ubia kati ya SUMA JKT na kampuni ya ANIT ASFALT ya Uturuki kwa mtaji wa shilingi Bilioni Tano na milioni mia moja ambapo SUMAJKT inamiliki asilimia 30 sawa na shilingi Bilioni moja na milioni mia sita na themanini.

(Picha na Freddy Maro)

Leave A Reply