The House of Favourite Newspapers

Rais Kikwete Na Mama Salma Kikwete Watoa Pole Kwenye Msiba Wa Balozi Mstaafu na Waziri wa zamani Dk. Deodorus Kamala

0

Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa pole nyumbani kwa Balozi Mstaafu na Waziri wa zamani Wizara ya Afrika Mashariki Dk. Deodorus Buberwa Kamala aliyefariki dunia Jumatatu Januari 12, 2024 katika hospitali ya Mzeena, Kijitonyama, Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Dk. Kamala, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 55, amewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Nkenge wilaya ya Missenyi mkoani Kagera kuanzia mwaka 2000 hadi 2010, na mwaka 2006 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afrika Mashariki na baadaye Waziri Kamili wa wizara hiyo mwaka 2008 hadi 2010

Mwaka 2011 aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Uholanzi ambako alitumikia nafasi hiyo hadi mwaka 2015 aliporejea kuwa Mbunge hadi mwaka 2020.

Leave A Reply