The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli Amtumbua Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli ametengua Rasmi nafasi ya Mtendaji Mkuu wa shirika la Elimu Kibaha, Dkt. Crispin Mpemba ili kupisha uchunguzi wa Tuhuma mbalimbali za kiutendaji zinazomkabili.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Rebecca Kwandu Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini Kutoka Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa imeeleza kuwa kwa sasa nafasi hiyo inakaimiwa hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.

 

Comments are closed.