The House of Favourite Newspapers

Bwana Misosi: Tangu Nitoke Vipi Mpaka Ufundi Umeme!

GABRIEL NG’OSHA | CHAMPIONI| Dar es Salaam

BWANA Misosi ambaye alikuwa hasikiki kwa muda kutokana na majukumu mengine, ameibuka na wimbo wake mpya wa Makofi kwa Magufuli. Bwana Misosi aliitikisa vilivyo nchi kwa nyimbo zake za Nitoke Vipi aliomshirikisha Hard Mad na Mabinti wa Kitanga aliomshirikisha Mwana FA, lakini kamanda huyu alikuwa kimya kwa muda mrefu kabla ya hivi karibuni kutoka na ngoma ya Makofi kwa Magufuli.

Kilinge ilifanikiwa kumtafuta, ikampata kisha ikafanya mahojiano na Bwana Misosi kuhusu harakati zake za muziki kwa sasa:

UNA KIPI KIPYA KWA SASA KWENYE MUZIKI?

Nimejipanga kurudi upya ndiyo maana nimeamua kuachia project ya Makofi kwa Magufuli, na mwakani nitaachia ngoma kibao tu.

ULIPOKU WA KIMYA, UMEJIFUNZA NINI KATIKA MUZIKI WA KIBONGO?

­­­­­­­Tulianza muziki kiaina bila faida, ila kwa sasa muziki ni biashara, kikubwa ni kufanya kazi nzuri, kujituma katika kutafuta soko la kimataifa.

MUZIKI UMEKUNUFAISHA VIPI?

Mafanikio ni mengi, pia nimeajiri kupitia taaluma yangu ya umeme (electrician). Nina fun base (mashabiki) kubwa na mambo mengi yanakuwa mepesi, kiujumla maisha ya

naendelea naendelea, yote kupitia muziki.

NINI KILICHANGIA KUKUPOTEZA KWENYE GEMU?

Wabongo wanashangaza sana, wasipokusikia au kukuona na ngom a mpya basi wanahisi umepotea, tangu awali sikuwa na kasumba ya kutoa ngoma mara kwa mara, kwani naami ni muziki wangu si Big G, ni muziki mkali unaoishi kwa muda.

NJE YA MUZIKI UNAFANYA ISHU GANI NYINGINE?

Kitaaluma, mimi ni fundi umeme, nina kampuni yangu ya Jefbemac Company ambayo inachukua tenda za kufunga umeme kwenye

makampuni na majumba mbalimbali, hivyo natumia muda mwingi kuiboresha zaidi kwani inanipatia ugali nje ya muziki.

UMEOA? KAMA NDIYO UMEBARIKIWA KUPATA MTOTO AU WATOTO WANGAPI?

Sijaona ila nina mchumba, muda wa Mungu ukifika nitamtambulisha tu. Sina mtoto wala watoto. MCHUMBA

WAKO ULIMCHAGUA KWA SIFA

ZIPI? Uzuri wa mwanamke si sura hata wazee wetu walisema hilo, nikisema hivyo unanielewa, nachomaanisha kwangu ni tabia njema, upendo kwangu na ndugu zangu, pia maelewano.

NANI ANAKUOGOPESHA KWENYE GEMU KWA KIZAZI KIPYA?

Hakuna hata mmoja, muziki ni uleule, ingawa muziki wa sasa kukopi kwa sana, na ninaamini kila mtu ana riziki yake.

UNAHISI WIMBO HUU UTAKURUDISHA KWENYE GEMU?

Kujiamini kunaanzia kwa mtu mwenyewe, ninaamini natoboa na siyo kwamba unanirudisha, mimi kwenye gemu bado nipo, na siku zote anayejua kupigana havui shati.

KWA NINI, MAKOFI KWA RAIS MAGUFULI?

Ujue wimbo wangu unawakilisha mamilioni ya Watanzania ambao wanamkubali kutokana na utendaji wake, kwa kuwa mimi ninaweza kuwasemea, ndiyo maana nimeamua kuwawakilisha.

NANI MPISHI WA NGOMA YA MAKOFI KWA MAGUFULI?

Hiyo imepikwa na mtayarishaji matata, Zest Mkali wa Studio ya Mojamoja Record, nikiwa nimemshirikisha mkali wa RnB, Nuruely

UNATAMANI KUFANYA KOLABO NA MSANII GANI WA KIZAZI KIPYA?

Msanii yeyote mwenye kipaji, na nimeishafanya kolabo kibao sana na wasanii wakali chipukizi ila hawafahamiki, na siyo lazima kufanya kolabo.

BAADA YA MAKOFI KWA MAGUFULI NINI KINAFUATIA?

Ndani nina maktaba ya ngoma kama 12 hivi, ambazo sijaziachia, ila Makofi kwa Magufuli inafanya vizuri na tayari nimefanya mahojiano sehemu nyingi hadi nchini Kenya.

NGOMA YAKO YA MWISHO ILIFANYA VIZURI?

Ndiyo, iliitwa Tungi na Misosi ambayo niliitoa mwaka 2013, nilimshirikisha Dullayo, ilinipa shoo baadhi.

MASHABIKI WAKO UNAWAAMBIA NINI KUHUSU UJIO WAKO MPYA?

Nimekuwa nikifanya kazi nzuri na wao kunishika mkono, bado nahitaji baraka zao ili niweze kuwaburudisha zaidi.

Comments are closed.