The House of Favourite Newspapers

RAIS MAGUFULI AMWAGA MABILIONI UHAMIAJI – VIDEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, leo amezindua hati mpya za kusafiria za kielektroniki, tukio lililofanyika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam na kutoa Tsh. Bilioni 10 kwa ajili ya kujenga makao makuu ya idara hiyo mjini Dodoma.

Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa pia na makamu wa rais na viongozi wengine mbalimbali wa kitaifa, waliostaafu na waliopo madarakani, Waziri Magufuli ameipongeza idara ya uhamiaji kwa jitihada wanazoendelea kuzifanya, na kueleza kuwa hati mpya itakuwa na manufaa mengi kwa kila Mtanzania.

 

Rais Magufuli amesisitiza kwamba, hati hizo mpya zitaanza kutolewa kwa gharama ya shilingi laki moja na elfu hamsini tu, hivyo hakuna mtu anayetakiwa kulipa zaidi ya kiwango hicho.

“Vibali vya ukaaji na uraia vya nchi yetu vilikuwa ninagawiwa bila utaratibu, wengine walipewa hadi vyeo vya juu kabisa serikalini wakati si Watanzania, mapato katika idara hii ya uhamiaji yalikuwa yanapotea.

“Idara ya uhamiaji ni nyeti lakini kuna kipindi imekuwa na mambo ya ajabu na ndio maana nilibadilisha uongozi uliokiwepo. Nina imani na Kamishna Anna Makakala, najua ni mwaminifu na ataifanya kazi inavyotakiwa. Nitatoa fedha shilingi Bilioni 10, mkatafute eneo Dodoma kwaajili ya kujenga makao makuu yenu

“Gharama za mradi huu kama ilivyoelezwa na kamishna mkuu wa uhamiaji ni USD milioni 57.82 sawa na shilingi Bil 127.2. Awali ilikuwa ufanyanyike kwa USD milioni 226 sawa na shilingi Bil 400. Walipanga kutupiga kwenye pesa ya Watanzani.

“Fedha zote za mradi huu zinatolewa na serikali ya Tanzania, na kama mnavyojua serikali inapata fedha kutokana na kodi zenu. Kwahiyo hongereni sana watanzania wa kulipa kodi,” alisema Rais Magufuli.

Fuatilia LIVE kupitia application ya Global Publishers na Global TV Online.

 

Comments are closed.