The House of Favourite Newspapers

‘SHUSHUSHU’ ALIYEPOTEZA MIKONO, MIGUU, UTUMBO KULIPWA BIL 245

OFISA wa ujasusi (shushushu) katika jeshi la Marekani, Lisa Maria Carter, wa Florida, Marekani, anajitayarisha kulipwa Sh. bilioni 245 (Dola milioni 109 za Marekani) kutokana na kufanyiwa vibaya oparesheni ya kutibu uvimbe uliokuwa umejitokeza katika sehemu ya uzazi mwaka 2010.

Lisa Maria Carter alivyo sasa.

Hivi sasa, Carter anabidi ahudumiwe kila kitu kutokana na athari aliyopata kutokana na oparesheni hiyo.

 

Mwaka huo, mwanamke huyo akiwa na umri wa miaka 45, alikuwa aondoke kwa ndege  kwenda Iraq kukusanya habari za ujasusi ambapo aliambiwa alikuwa na uvimbe kwenye sehemu ya uzazi (ovarian cyst).

…Anavyotembea kwa kutumia nyenzo maalum

Katika oparesheni iliyofuata ya kumtibu, ambayo ilifanyika vibaya, ilisababisha apoteze mikono yake yote, miguu, utumbo na misuli ya tumbo.  Hii ilitokana na kumsababishia kukumbwa na bacteria zilizoula mwili wake na kuharibu sehemu mbalimbali.

…Akiwa na mtaalam wa tiba

Katika upasuaji huo, shinikizo lake la damu lilishuka sana na kuathiri mzunguko wa damu mwilini ambapo pamoja na madaktari kumpatia damu mfululizo, mikono na miguu yake vilikufa kutokana na kutopata damu, hivyo madaktari kuamua kuvikata.

 

Matokeo yake, mama huyoambaye sasa ana umri wa miaka 53 anahitaji kusaidiwa kwa kila kitu kwani hawezi kutembea ambapo viungo vya usagaji wa chakula (utumbo) vimewekwa katika  mfumo maalum nje ya tumbo lake.

 

Hivi  majuzi, mahakama moja nchini Marekani ilisema kwamba Chuo Kikuu cha South Florida, kilichokuwa kimemwajiri daktari aliyehusika na oparesheni hiyo iliyofanywa vibaya, kinalazimika kumlipa mama huyo Dola milioni 109.

 

Imesemwa kwamba kilichomsababisha mama huyo kupoteza viungo hivyo kwa miaka minane sasa, ni daktari mmoja kukata kimakosa sehemu ya tumbo iliyovujisha bacteria wenye kula nyama (mwili wa mtu), ambao walishambulia mwili wa mwanamke huyo.  Bakteria hao wakiwa ndani ya eneo husika la tumbo, huwa hawana madhara

 

Carter  hivi sasa anatembea kwa kutumia pikipiki maalum na anatumaini kufanyiwa oparesheni kurudishiwa viungo vya mwili wake.

WALUSANGA NDAKI/MITANDAO/MASHIRIKA YA HABARI

Comments are closed.