The House of Favourite Newspapers

JPM Arudisha Fomu za Urais, Apata Wadhamini Kibao -Video

0
Rais John Pombe Magufuli.

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais John  Magufuli, ambaye ni mgombea urais kupitia chama hicho amerudisha fomu za kugombea nafasi hiyo leo Juni 30, 2020, jijini Dodoma, katika ofisi kuu za chama hicho.

 

Akiongea baada ya kupokea fomu hizo,  Katibu mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amesema kuwa,  Magufuli amedhaminiwa na wanachama 1,023,911 Tanzania nzima.

 

Ameongeza kuwa kikao cha Kamati Kuu kitakaa Julai 10, 2020, ili kupitisha majina ya wagombea urais, Tanzania na Zanzibar.

Katibu mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally

Baadhi maneno aliyosema Magufuli ni haya:

“Nawashukuru sana Wenyeviti wa Mikoa yote mliamua ninyi wenyewe kwamba hizo fomu za wadhamini niwaletee ili mimi nisihangaike kuzunguka kila mahali, mmepata lawama watu wengi walitaka kudhamini lakini karatasi zikawa zimepungua ninaomba radhi sana kwa hilo.
“Tarehe 17 mwezi uliopita niliamini kabisa kwamba, uchukuaji fomu wangu uwe kama kawaida yangu, nilijitahidi kuwatoroka vizuri sana, Katibu Mkuu akawa ananiuliza utakuja lini? Alipanga  saa 5 mimi nikaja saa 2 nikachukua fomu nikaondoka.
“Najua changamoto za uongozi ni ngumu sana, zina mateso sana. Jana nimetoka Kilosa saa mbili, nimekuta mambo mezani, nimelala masaa matatu na nimelala peke yangu lakini kikubwa ni mimi nawashukuru sana.
“Niwaombe sana hasa wagombea wa CCM upande wa Zanzibar wawe waangalifu wasiumizane kwenye kunadi sera zao maana kazi sio urais tu. Hata kwenye majimbo watia nia mtarogana bure na kuumizana bure kwani atakayechaguliwa Mungu anamjua.
Nimeambiwa watia nia katika majimbo mengine wako zaidi ya 20, mtaragona, mtaumizana bure. Atakayechaguliwa ni mmoja tu. Kuanzia kesho tarehe moja mwenzi wa saba ruksa wana-CCM kupitapita ofisini kuchukua fomu kuomba ridhaa ya kuwania nafasi za uongozi.
”Tukigombana wakati wa kampeni tutapoteza direction (mwelekeo). Atakayechaguliwa wakati wa kampeni tumbebe. Nafasi zipo nyingi za kuteua na hata sasa zipo kama nne sijateua. Najiuliza nimteue nani? Muhimu ni tushike dola kwanza.”

Leave A Reply