The House of Favourite Newspapers

JPM Atoa Siku 30 Viongozi Kumsimamia Mkandarasi – Video

0

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Eng. Isack Kamwelwe pamoja na viongozi mbalimbali akiweka jiwe la msingi Ujenzi wa Barabara ya Dumila-Kilosa-Mikumi sehemu ya Rudewa-Kilosa Km 24 katika sherehe zilizofanyika katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro.

RAIS  John Magufuli ametoa siku 30 kwa viongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kumsimamia usiku na mchana mkandarasi wa kampuni ya Padiel JV kuhakikisha anakamilisha kwa haraka kazi ya ujenzi wa barabara ya Kilosa- Dumila yenye urefu wa kilometa 24.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na baadhi ya Mawaziri, wakuu wa Mikoa, viongozi mbalimbali, akikata utepe ili kuzindua mitambo itakayotumika katika ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro.

Akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara hiyo jana (Jumatatu Juni 29, 2020), Magufuli alisema hajaridhishwa na mwenendo wa  utekelezaji wa mradi huo unayofanywa na mkandarasi huyo kutokana ujenzi wa barabara hiyo kuchukua muda mrefu kukamilika.

 

Alisema kumekuwepo na malalamiko ya makampuni mengi ya kizalendo kuhusu kutopewa kazi za miradi ya serikali, lakini pindi yanapopewa,  kazi hizo yameshindwa kutekeleza ujenzi wa miradi hiyo, hatua inayosababisha kuchelewesha maendeleo ya wananchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mawaziri, baadhi ya Viongozi wa Serikali, katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni zinazojenga mradi wa Reli ya Kisasa SGR Kilosa mkoani Morogoro.
Sehemu ya Handaki kubwa lenye urefu wa Kilometa 1.1 ambalo litapitisha treni hiyo katika eneo la milima ya Kilosa mkoani Morogoro.



Aidha alimtaka Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe,   na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD) kuhakikisha kuwa iwapo kuna vikwazo vinavyokwamisha utekelezaji wa ujenzi wa barabara hiyo ikiwemo malipo,  yashughulikiwe haraka.

 

‘’Sifurahishwi na kazi ya mkandarasi,  ningekuwa mimi ni Kamwelwe (waziri) basi leo asingekuwepo huyu mkandarasi, haiwezekani tuwape kazi halafu ifanyike ya hovyo hivi, natoa rai kwa makandarasi wote wanaotekeleza miradi ya ndani wabadilike,’’ alisema Rais.

 

Aliongeza kuwa katika kipindi cha uongozi wake, serikali ya swamu ya tano kamwe haitawatetea wakandarasi wazembe na kuitaka kampuni ya Padiel JV kuhakikisha ujenzi wa barabara hiyo unakamilika haraka kwa kuwa kwa kipindi kirefu wananchi wa Wilaya ya Kilosa wamekuwa wakiishi katika mateso makubwa ya barabara hiyo.

 

Aidha aliiagiza Wakala wa Barabara Nchini Mkoa wa Morogoro kuanza kufanya usanifu na upembuzi yakinifu wa kipande cha barabara iliyosalia ya Kilosa-Mikumi yenye urefu wa Kilometa 70 ili kipande hicho kiweze kukamilika kwa haraka.

 

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa TANROAD, Mhandisi Patrick Mfugale,  alisema ujenzi wa barabara hiyo inayounganisha Wilaya ya Handeni (Tanga)-Turiani-Dumila-Kilosa-Mikumi, una gharama ya kiasi cha Tsh. Bilioni 32 na kukamilika kwake kunatarajia kupunguza changamoto ya usafiri.

Leave A Reply