The House of Favourite Newspapers

RAIS MAGUFULI ATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA QURAAN (PICHA +VIDEO)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli akimzawadia Mohamed El Moujabba Diallo wa Senegal baada ya kuzoa Alama 99.88 na kuibuka Mshindi wa Kwanza wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalum ya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar, leo Jumapili Mei 19, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli akimzawadia Sumayyah Juma Abdallah wa Tanzania baada ya kupata alama 98.66 na kuibuka Mshindi wa Tano wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalum ya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar, leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli akimzawadia Idrissa Ousmane wa Niger baada ya kupata alama 98.67 na kunyakua ushindi wa nne wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalum ya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar, leo Jumapili Mei 19, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli akimzawadia Shamshuddin Hussein Ali wa Zanzibar baada ya kuzoa alama 98.83 na kuibuka Mshindi wa Tatu wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalum ya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar, leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya waumini wa Kiislam na wadau wengine wakati akihitimisha mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar, leo.

PICHA NA IKULU

Rais wa Tanzania, John Magufuli ametoa zawadi mbalimbali za washindi wa mashindano ya 20 ya kusoma na kuhifadhi Quran Afrika yaliyofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar, leo.

Katika hotuba yake, Magufuli amesema anafahamu uwepo wa watu wenye tamaa ya kupandisha bei katika kipindi cha Mfungo wa Ramadhani hivyo amewataka kuacha tabia hiyo mara moja.

Amesema kufanya hivyo ni dhambi mbele ya Mwenyezi Mungu kufanya hivyo hakuwezi kumtajirisha mtu hasa kwa kupandisha bei ya vile vitu vinavyotumika sana katika mfungo huu.

“Nitumie fursa hii kutoa wito kwa mamlaka husika za Serikali kufuatilia suala hili kwa ukaribu sana,” amesema Magufuli.

Mbali na hilo amewataka watu wa madhehebu mengine na wale wasiokuwa na dini kuendelea kushirikiana na Waislam katika kutimiza mfungo wa mwezi huu ambao ni moja ya nguzo tano za Uislam.

“Namuomba Mungu awalipe malipo stahiki juu ya kile mnachokifanya katika funga zenu. Mimi mwenyewe sijafunga, lakini siku ya kufumgua Waislam nitakua nanyi katika pilau,” amesema.

Rais MAGUFULI Anazungumza Muda Huu TAIFA Kwenye Mashindano Ya Quraan

Comments are closed.