The House of Favourite Newspapers

JPM ATOA POLE KWA SHIGONGO KUFIWA NA MAMA YAKE

Rais John Magufuli akisaini kitabu cha maombolezo.

RAIS  John Magufuli na  mkewe Janeth, wamejumuika na watu mbalimbali kumpa pole Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, aliyefiwa na mama yake mzazi, Bi. Asteria Kahabi Kapela, alfajiri Ijumaa, Julai 27, 2018 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akitibiwa.

Msiba huo upo nyumbani kwa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Eric Shigongo (kulia) akimpolea Rais  Magufuli.

Wakibadilishana maneno kadhaa.

Mama Janeth, Rais Magufuli na Shigongo wakielekea walikokuwa waombolezaji wengine.
…Wakisalimiana na waombolezaji.

PICHA: MUSA MATEJA , GPL

Comments are closed.