The House of Favourite Newspapers

Magufuli: Machinga, Mama Ntilie Wasifukuzwe Stendi – Video

0

RAIS  John Magufuli amezindua Kituo Kikuu cha Kimataifa cha Mabasi cha Dar es Salaam, kilichopo Mbezi-Luis, leo Jumatano, februari 24, 2021, kikiwa na uwezo wa kuhudumia mabasi 3,456, abiria 224,000, uwezo wa kuegesha magari madogo zaidi ya 280, mabasi 1,000 —  yote hayo kwa siku.

 

Amesema amefurahi Dar es Salaam kuchagua wabunge wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jambo ambalo alitamani litokee ili kusukuma haraka maendeleo katika jiji hilo huku pia akiziagiza mamlaka zinazosimamia soko hilo kutowabughudhi wafanyabiashara wadogowadogo kwani stendi hiyo imejengwa pia kwa ajili yao kujipatia kipato na si kwa watu fulani tu.

 

 

“Ukigeuka kule kuna Mtemvu, kule kuna Zungu, ukigeuka huku Chaurembo, jamani mnisamehe kama nimefanya kosa CCM Oyee, hii ndiyo nchi ninayotaka kuijenga, unapokuwa kiongozi ni lazima upate watu wanaowakilisha watu.

 

“Mtemvu ameomba Heka 52, Mimi nakupa kwasababu hauziombi kwa ajili ya kujenga nyumba yako unaziomba kwa ajili ya Wananchi hawa wanyonge, nakupa hiyo zawadi ya Heka 52 bure ukaziendeleze kwa ajili ya Wananchi, Kibamba hamkukosea kuchagua.

 

“Nimeshangaa Jafo kuandika Stand hii ya Mbezi Luis kwa jina langu maana angeweza kuandika Jafo Stand, sifurahii sana majina yangu kutumika kwasababu naogopa kitu kimoja, mnaweza kuandika jina langu halafu Wananchi masikini Wamachinga n.k, wakawa wananyanyaswa hapa.

 

 

“Mimi nilichaguliwa na Wananchi hawa wanyonge lakini mara nyingi vitu hivi vizuri vikikamilika Wamachinga wanafukuzwa, Watu wa kawaida wanafukuzwa, nitaumia sana kama Wananchi hawa wanyonge watakuwa wanafukuzwa halafu mmeandika Stand ya Magufuli.

 

 

“Mkiwafukuza Wamachinga hapa wakati Stand imeandikwa Stand ya Magufuli itaonesha Magufuli ndiye anawafukuza, sitokubali, nikueleze Waziri Jafo inawezekana umejichongea kwa kuiita Stand hii Magufuli, nataka yafanyike ambayo mimi Magufuli nataka.

 

“Nilikuwa naangalia Katibu Mkuu akieleza yaliyomo humu, kuna Ofisi ya Uhamiaji haimsadii mmachinga, kuna Hoteli na Gesti inawezekana Mmachinga asiingie, mmeipa Stand jina langu ngoja nikubali ili kuwatetea hawa watu, nataka niwe Balozi wao, hawa Wamachinga wasifukuzwe hapa.

 

 

“Wamachinga watengenezewe utaratibu, abiria wakanunue chakula kwa wamachinga, wenye hela nyingi ndiyo waende kwenye hotel, viazi, mihogo na matikiti maji nayo yanunuliwe hiyo ndiyo serikali inayojali wananchi wake.

 

 

“Wananchi hawa wanyonge wasifukuzwe hapa (Stand ya Magufuli) muwatengenezee utaratibu, kama kutakuwa na Mabasi 3000 yanaingia hao abiria wakanunue chakula kwa Wamachinga, wenye hela nyingi ndio wakale Hotelini, lakini hata mihogo ya Mama Lishe inunuliwe.

 

“Waziri Jafo ungeiita hii Stand Jafo au jina jingine Mimi wala nisingejali, lakini umeiita jina la Magufuli, wafa, najua hii ni challenge kwa viongozi mtaaanza kujiuliza hapa tutafanyaje, mjipange kwa namna gani Wamachinga na Mama Lishe watanufaika kwa hii Stand mpya.

 

 

“Nilipokuja mwaka jana nilikuja hapa na Rais wa Malawi, siku hiyo sikufurahia kwasababu hata gharama ya fedha za ujenzi ziliongezeka karibu Bilioni 20, leo umezungumza juu ya Bilioni 50.95 nimefurahi na nawapongeza sana mlioshiriki.

 

“Stand hii ni ya Kimataifa kwa sababu itapokea mabasi na wageni kutoka nchi jirani, ningeomba isihartibiwe, isichorwechorwe, ibaki na hadhi ya Kimataifa,” amesema Magufuli.

 

 

Leave A Reply