The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Rais Magufuli Awasili Jijini Arusha (LIVE)

0

 

RAIS John Magufuli leo Jumatano amewasili jijini Arusha kwa ziara maalumu ya siku tatu ambapo mapema asubuhi atafungua barabara ya Kami  kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) hadi Mererani wilayani Simanjiro.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alisema Rais Magufuli anatarajiwa kupokewa uwanja wa ndege wa Kilimanjaro saa mbili asubuhi.

Gambo alisema  baada ya kupokelewa atakwenda Mererani Mkoa wa Manyara kuzindua barabara ya Kia-Mererani yenye urefu wa kilomita 26.

Amesema baada ya uzinduzi huo atazungumza na wananchi na baadaye kurejea Arusha. Gambo amesema Rais Magufuli anatarajiwa kutoa kamisheni kwa maafisa waliohitimu mafunzo ya jeshi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jumamosi.

“Napenda kutumia fursa kuwaomba wakazi wa Arusha kujitokeza Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Septemba 23 kuanzia saa 12:30 asubuhi,” alisema.

RPC Arusha Aweka Wazi Usiyoyajua Kuhusu Aliyewateka na Kuwaua Watoto Arusha

Leave A Reply