Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete Afanya Mazungumzo na Rais wa Kenya William Ruto

Rais Mstaafu was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Novemba 19, 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kenya, William Samoei Ruto, Ikulu, Nairobi.
Rais Mstaafu Kikwete ambaye ni Mlezi wa Jukwaa la Vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (YouLead Summit) pamoja na mambo mengine, alifika Ikulu ya Nairobi kumjulisha Mheshimiwa Rais Ruto juu ya masuala mbalimbali ya Mkutano wa Jukwaa hilo unaotarajiwa kuanza leo jijini Nairobi.