The House of Favourite Newspapers

Rais Mwinyi Atumbua Watano

0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametengua uteuzi wa viongozi watano wa idara na wizara mbalimbali, kuanzia leo, Februari 3, 2022 akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utumishi na Uendeshaji katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

 

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Mhandisi Zena Said imewataja wengine waliotenguliwa kuwa Suleiman Yahya Ame aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na Fatma Iddi Ali aliyekuwa Kamishna wa kazi katika Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji.

 

Wengine ni Salum Ubwa Nassor aliyekuwa Afisa Mdhamini, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Nasima Haji Choum aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia na Watoto katika Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto.

Leave A Reply