The House of Favourite Newspapers

Mradi wa Maji Kichefuchefu Wamchefua Shigongo

0

MBUNGE wa Buchosa, Mhe. Eric Shigongo ametaka majibu ya Serikali kuhusu mradi mkubwa wa maji Lumeya, Nayakaliro, Kalebezo hadi Nyehunge ambao umegharimu Zaidi ya Tsh bilioni 1.6 huku ukiwa umejengwa chini ya kiwango.

 

Akizungumza Bungeni leo, Mhe Shigongo amesema mradi huo ni kichefuchefu kwani umegharimu pesa nyingi za serikali lakini kwa kuwa umejengwa chini ya kiwango, mabomba yanapasuka na wananchi hawapi maji kabisa huku akimuomba Waziri mwenye dhamana ya Maji kufika katika mradi huo ili kujionea mwenyewe namna ambavyo mradi huo umekuwa kero kwa wananchi wa Buchosa.

 

Aidha, Mhe Shigongo ameiomba Serikali kupeleka wachunguzi maalum ili kubaini ubadhirifu na kuwachukulia hatua wote waliohusika kufanya mchezo huo mchafu.

 

Kwa Upande wa Serikali kupitia Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Meryprisca Mahundi amesema tayari Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameshaunda kikosi kazi ambacho kinachunguza miradi yote kichefuchefu na kuhakikisha inashughulikiwa na wananchi wanapata maji huku wahusika wa ubadhirifu huo wakichukuliwa hatua za kisheria.

Leave A Reply