The House of Favourite Newspapers

Rais Mwinyi Kufanya Ziara ya Kikazi Nchini China

0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar kuelekea jijini Dar es Salaam tayari kwa safari ya ziara ya kikazi nchini China.

 

Rais Dkt. Mwinyi akiagana na viongozi

Katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume Rais Dk.Mwinyi ameagwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla.

Rais Dk.Mwinyi ameambatana pia na mkewe Mama Mariam Mwinyi na pamoja na viongozi mbalimbali .

 

Viongozi wengine waliomuaga Mhe.Rais Dk.Mwinyi ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustapha, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Mstahiki Meya wa jiji la Zanzibar Mahmoud Mohammed Mussa Balozi mdogo wa China anaefanyia kazi zake Zanzibar Zhang zhisheng akimwakilisha Balozi wa China nchini Zanzibar, Wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama wa SMZ na SMT pamoja wa viongozi wa Chama.

 

Leave A Reply