The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Achanjwa Chanjo Ya Corona Hadharani Leo Ikulu Dar (Picha +Video)

0

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, leo Julai 28, 2021, amechoma chanjo Johnson & Johnson inayotolewa kwa dozi moja tu, ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona ambapo amesema kuwa amefanya hivyo kwa hiari yake mwenyewe baada ya wanasayansi kujiridhisha na usalama wa chanjo hiyo.

Kauli hiyo ameisema leo Ikulu ya Dar es Salaam, ambapo amesisitiza kwamba yeye ni Mama, Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, Bibi na mke pia, hivyo asingejipeleka mwenyewe kwenye kifo licha ya kuwa na majukumu mengi kwenye Taifa.

 

Mimi ni mama, mke, Rais na Amirijeshi Mkuu nisingejitoa mwenyewe kujipeleka kwenye hatari huku nikijua kwamba nina majukumu yote hayo, nimekubali kwa hiari yangu kuchanjwa kwani sioni hatari iliyopo kwasababu tayari wanasayansi wamejiridhisha”

 

“Chanjo ni hiari na pia ni imani kwa wale wenye imani potofu tutaendelea kuwapa elimu. Pamoja na chanjo naomba tuendelee kuchukua tahadhari”

 

“Niwahakikishie Watanzania kuwa tutahakikisha chanjo inapatikana kwa wale wote ambao kwa hiari yao wako tayari kuchanja”

 

“Chanjo tulizonazo ni kidogo ukilinganisha na idadi ya Watanzania, na wengi wanaikubali hivyo jitihada za kuongeza chanjo hii zinaendelea kufanyika” – amesema Rais Samia

Leave A Reply