The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Afanya Mabadiliko Baraza la Mawaziri, Simbachawene, Mhagama Wabadilishana Wizara

0

Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kwamba Rais Samia amemteua Jenista Mhagama kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), akichukua nafasi ya George Simbachawene.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Rais Samia amemteua George Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, akichukua nafasi ya Mhagama, uteuzi ambao umeanza leo, Aprili Mosi, 2023.

Mawaziri wateule wataapishwa kesho, Aprili 2, 2023, saa 3 asubuhi, ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Leave A Reply