The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Afanya Uteuzi wa Mkuu Mpya wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF)

0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amempandisha Cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali na amemteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (Chief of Defence Forces-CDF)

Wakati huohuo Rais Samia amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi aliyemaliza muda wake Jenerali Venance Salvatory Mabeyo  alipokwenda kumuaga Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo. Jenerali Mabeyo alifika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumuaga Mhe. Rais Samia wakati akimaliza kipindi cha Utumishi wake katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
Leave A Reply