The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Afunga Mafunzo Ya Uofisa Chuo Cha Polisi Kurasini Dar- (Picha+Video)

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Cheti cha Heshima kwa Mhitimu aliyefanya vizuri katika Medani za Kivita PF 18911 ASP Evelyne Mathias Msobi katika Mahafali iliyofanyika leo tarehe 12 Desemba 2021katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Cheti cha Heshima kwa Mhitimu aliyefanya vizuri katika nidhamu PF 17874 ASP Ally Juma Mwapumba kati ya Maofisa Wanafunzi wapya wa mafunzo ya Uofisa Kozi No. 1/2021 katika mahafali yaliyofanyika leo tarehe 12 Desemba 2021katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa maofisa wa Jeshi la Polisi Tanzania. Hafla hiyo inafanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo Kurasini mkoani Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki katika Mahafali ya Kufunga Mafunzo ya Uofisa Kozi No. 1/2021 leo Jumapili Desemba 12, 2021 katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini, Jijini Dar es Salaam.

Jumla ya maofisa 747 wamehitimu mafunzo hayo.

Leave A Reply