The House of Favourite Newspapers

Uzinduzi Wa Matangazo Ya Vivutio Vya Utalii Katika Mabasi Nchini Israel

0
Balozi wa Tanzania nchini Israel, Job Masima akikata utepe kuashiria uzinduzi wa matangazo ya vivutio vya utalii katika mabasi ya abiria yanayofanya safari zake kati ya jiji la Tel Aviv na miji ya jirani nchini Israel.

Katika kuhitimisha maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Job Daudi Masima, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Israel amezindua matangazo ya vivutio vya utalii katika mabasi ya abiria yanayofanya safari zake kati ya jiji la Tel Aviv na miji ya jirani, katika stendi kuu ya mabasi, katika kitongoji cha Petach Tikva.

Matangazo hayo yamebandikwa kwenye mabasi yapatayo 125 kwa muda wa wiki tatu kuanzia tarehe 10 – 31 Disemba 2021. Matangazo hayo yanayoonesha Mlima Kilimanjaro; Wanyama katika hifadhi ya Serengeti; Ngorongoro na fukwe za Zanzibar yanatoa fursa kwa wakazi wa Israel kujionea vivutio hivyo na kuhamasika kutembelea Tanzania mara baada ya masharti ya UVIKO kulegezwa.

Leave A Reply