The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Akerwa na Kibanda cha TANESCO

0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezungumzia ubadhirifu wa fedha ambao umekuwa ukifanywa na Halmashauri na kugusia kibanda cha mlinzi cha Tanesco kilichojengwa kwa Sh7 milioni.

 

Wiki moja iliyopita akiwa ziarani Mkoa wa Kagera, Wilayani Kyerwa, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikataa kuzindua mradi wa ofisi ya Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco) kutokana na gharama zilizoamniika kuwa kubwa kuliko aina ya majengo yaliyopo ikiwemo kibanda hicho cha mlinzi.

 

Akizungumza leo Jumatatu Septemba 27,2021 katika mkutano mkuu maalum wa uchaguzi viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania(ALAT) ngazi ya Taifa unaofanyika mkoani Dodoma, Rais Samia pamoja na mambo mengine alizungumzia suala la ubadhirifu wa fedha katika Halmashauri na kutolea mfano ujenzi wa kibanda hicho.

 

“Juzi nilimuona Waziri Mkuu sijui alienda wapi akaenda akapelekwa kwenye kakibanda ambako ameambiwa kimejengwa kwa milioni kadhaa, lakini ukikaangalia kale kakibanda na thamani ya fedha ni tofauti.

 

“Kamepakwapakwa rangi vizuri mbele lakini ni kibanda ambacho kingejengwa kwa Shilingi milioni nne au tatu lakini mamilioni kadhaa yamemiminika pale.

 

Kwa hiyo lengo langu pamoja na kuleta fedha zitakazoendelea kuleta thamani ya miradi inayotekelezwa ionekane huo ndio wajibu wenu na liwe la kwanza katika utekelezaji wenu wa majukumu ya kazi,”amesema Rais Samia.

 

Leave A Reply