The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Akutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

0

Rais Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya siasa, Balozi Victoria Nuland, Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu inaeleza kuwa Balozi Nuland amemshukuru Rais Samia kwa kuendeleza ushirikiano na serikali ya Marekani ambapo amesema mwaka 2021 ushirikiano huo unatimiza miaka 60 hivyo kuomba uimarike zaidi.

 

Amesema Marekani itazidi kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha afya za Watanzania kwa kutoa misaada kama ilivyofanya kupitia mpango wa Covax ambapo uliisaidia Tanzania kupata dozi zaidi ya milioni moja za chanjo ya Corona.

 

Ameongeza kuwa mbali na eneo la afya, Balozi Nuland amesema serikali ya Marekani itaendeleza ushirikiano na Tanzania katika kuimarisha uwekezaji, biashara na masuala ya ulinzi.

 

Leave A Reply