The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Amuagiza Majaliwa Kuunda Kamati Mauaji Mtwara

0

Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuunda kamati huru kuchunguza tuhuma za mauaji mkoani Mtwara yanayodaiwa kufanywa na askari polisi.

 

Akizungumza leo Ijumaa Februari 4, 2022 wakati akiwa Magu akielekea katika sherehe za maadhimisho ya miaka 45 ya CCM mkoani Mara zitakazofanyika kesho, Rais Samia amekosoa polisi kuunda kamati ya kujichunguza wenyewe baada ya tukio hilo.

 

“Kuna mauaji yametokea Mtwara na kwa taarifa zilizopo ni Polisi ndio lililofanya mauaji. Taarifa niliyonayo ni kwamba Polisi wameunda kamati ya kufanya uchunguzi halafu walete taarifa.”

 

“Haiwezekani Jeshi lifanye mauaji halafu jeshi lichunguze lenyewe” amesema Rais Samia nakuongeza.

Leave A Reply