The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Amuapisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara na Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Ikulu Dar

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ndugu Maryam Ahmed Muhaji kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Desemba 20, 2023 amewaapisha Maryam Ahmed Muhaji kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara na George Nathaniel Mandepo kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ndugu George Nathaniel Mandepo kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.
Ndugu Maryam Ahmed Muhaji Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara na Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Ndugu George Nathaniel Mandepo wakiapa kiapo cha Maadili katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.
Rais Samia akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Pindi Chana, Kamishna wa Maadili Jaji, Sivangilwa Mwangesi, Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Ndugu Majula Mahendeka, Mkuu wa Mkoa Manyara, Queen Sendega na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,  Albert Chalamila katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala walioapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Tanzania Startup Association (TSA) ikiongozwa na Mwenyekiti wao Ndugu Paul Makanza pamoja na Wajumbe aliofuatana nao walipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.
Rais Samia akiwa kwenye mazungumzo na Tanzania Startup Association (TSA) ikiongozwa na Mwenyekiti wao Ndugu Paul Makanza pamoja na Wajumbe aliofuatana nao walipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.
Rais Samia akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Tanzania Startup Association (TSA) Ndugu Paul Makanza, Mtendaji Mkuu Ndugu Zahoro Muhaji na Makamu Mwenyekiti, Ndugu Lulu Ng’wanakilala pamoja na Wajumbe waliofuatana nao mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.

 

PICHA NA IKULU

NONDO za RC CHALAMILA kwa TRA ZILIZOWAVUNJA MBAVU WATUMISHI – “TUENDELEE KUWA WAKALI”..

Leave A Reply