The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Aongoza Kuaga Mwili wa Mhandisi Mfugale-Picha

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitoa salam za Serikali kwenye Hafla ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale katika viwanja wa Karimjee Jijini Dar es Salaam leo tarehe 02 Julai, 2021.

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameongoza waombolezaji katika ibada ya kuaga mwili wa  aliyekuwa mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), mhandisi Patrick Mfugale inayofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

 

Mfugale alifariki dunia Jumanne Juni 29, 2021 saa 5 asubuhi katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitoa Heshima za mwisho katika Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale katika viwanja wa Karimjee Jijini Dar es Salaam leo tarehe 02 Julai, 2021.

Mwili wa Mfugale unaagwa leo Ijumaa Julai 2, 2021 katika viwanja hivyo kabla ya kusafirishwa kwenda  Ifunda mkoani Iringa kwa mazishi yatakayofanyika nyumbani kwake Julai 5, 2021.

 

Kwa mujibu wa ratiba baada ya kutoa heshima ya mwisho, mwili wake utapelekwa nyumbani kwake Kimara Temboni,baada ya misa takatifu siku ya Jumamosi Julai 3, 2021 atasafirishwa kwenda Ifunda mkoani Iringa kwa ajili ya maziko yatakayofanyika Julai 5, 2021.

Leave A Reply