The House of Favourite Newspapers

IFC Yataja Mkurugenzi wa Mawasiliano Vodacom Kinara Sekta ya Huduma za Kifedha

0
Taasisi ya kifedha IFC imemtaja Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC,Rosalynn Mworia kuwa ni miongoni mwa wanawake 22 wanaofanya vizuri katika sekta ya huduma za kifedha hapa nchini.
Kwa Mujibu wa Ripoti ya Nguvu ya Usawa iliyotolewa hivi karibuni na Taasisi ya IFC ilimtaja Rosalynn kuwa miongoni mwa wanawake wanaotimiliza majukumu yao vizuri kama wanaume waliopo katika sekta ya utoaji huduma za kifedha huku yeye akifanya vizuri katika huduma ya M-Pesa.
Aidha ripoti hiyo ambayo ilimtaja Rosalynn ilieleza kuwa nguvu ya usawa barani Afrika inaweza kuongeza uchumi hadi asilimia 10 ifikapo mwaka 2025 iwapo wanawake watakuwa katika nafasi za mameneja,wajumbe wa Bodi au wafanyabiashara.
Mbali ya hayo ripoti hiyo imeonyesha kuwa Rosalynn ni mtengenezaji wa soko hususan kwa wateja wa M-Poesa ambao wanakadiriwa kufikia milioni 14 tangu ilipoanzishwa.
Akizungumzia juu ya ripoti hiyo ya usawa wa kijinsia ya IFC ,Rosalynn alisema ameipokea vizuri  ikizingatiwa kwamba mwanamke anao uwezo wa kiutendaji sambamba na kuibadilisha jamii  nzima.
Alibainisha kuwa sera zinazohusu jinsia ni muhimu ili kumuwezesha mwanamke kufanya kazi vyema ili kuboresha fursa za wanawake mahali pa kazi.
“Kizazi cha sasa ni cha wanawake hivyo ni lazima kuwepo majukumu katika kuboresha matarajio ya kazi ya mwanamke”alisisitiza Mworia.
Leave A Reply