The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Ashiriki Mkutano wa SADC Congo, Sekta ya Maji Yawa Sehemu ya Mjadala Mkuu

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yupo nchini Congo kushiriki mkutano wa 42 wa wakuu wa nchi na serikali ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) utakao fanyika Kinshasa nchini Congo.

 

Mkutano huo umebeba malengo ya maboresho na mapinduzi ya viwanda, maboresho ya kilimo, maboresho ya Sekta ya Maji na kukabiliana na matishio ya ugaidi katika ukanda wa SADC kwaajili ya maendeleo ya nchi wanachama

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Malawi Lazarus Chakwera

Mkutano huu unajiri wakati dunia ikikabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo kupanda kwa bei za bidhaa kuliko sababishwa na mzozo kati ya Urusi na Ukraini, mkutano huo unaenda kufungua milango kati ya nchi wanachama ili kukabiliana na matatizo hayo.

 

Katika mkutano huo Felix Tshisekedi Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) atachukua uenyekiti wa SADC kutoka kwa Rais Lazarus Chakwera wa Malawi.

 

 

Imeandikwa: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao

Leave A Reply