Rais Samia Atangaza Kuwajengea Nyumba Walioathirika Na Mafuriko Manyara, Atoa Maagizo (Picha +Video)
Rais Samia Suluhu Hassan, amesema wataalam wa serikali, tayari wametenga eneo ambalo litatumika kuwahamisha waathirika wa maporomoko ya tope, Hanang mkoani manyara ambapo itawaunga mkono katika ujenzi wa makazi mapya ya kudumu.
Pia amezitaka taasisi za serikali kuwa na utaratibu wa kuchunguza kwa makini majanga ya asili kabla hayajatokea na kuchukua tahadhari ili kuepusha madhara kama yaliyotokea Hanang.