The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Atia Neno Ushindi wa Ruto Kiti cha Urais Kenya

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

BAADA ya Tume Huru ya Uchauzi ya Kenya IEBC hapo jana tarehe 15 Agosti 2022 kumtangaza Dkt. William Ruto kuwa mshindi wa kiti cha Uraisi akimshinda mpinzani wake wa karibu Bwana Raila Odinga na hivyo kuwa mrithi wa kiti cha uraisi Kenya kutoka kwa mtangulizi wake Mh. Uhuru Kenyata.

 

Leo hii Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pongezi kwa Wakenya wote kwa uchaguzi wao walioufanya kwa Amani na utulivu uliopelekea kupatikana kwa Rais mteule kupitia tiketi ya chama cha UDA Dkt. William Ruto.

 

Kwa upande mwengine Rais Samia ameahidi kudumisha umoja na ushirikiano wa kihistoria uliodumu kwa muda mrefu kati ya hizi nchi mbili za Kenya na Tanzania.

Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya William Ruto

Kwa mujibu wa Katiba ya Kenya, baada ya mshindi wa nafasi ya Urais kutangazwa na kusipokuwa na pingamizi la ushindi wake, basi Rais huyo mteule ataapishwa siku 14 baada ya siku ya kutangazwa kwake. Hivyo Dkt. Ruto anatarajiwa kuapishwa siku ya tarehe 30 Agosti 2022.

 

Imeandikwa: Abdallah Kaputi kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply