testiingg
The House of Favourite Newspapers

Zamu ya Hamisa Kutesa na Range Rover Lenye Thamani ya Shilingi Milioni 150

0
Mwanamama staa wa muziki, filamu na mitindo nchini Tanzania, Hamisa Mobeto.

 

Hamisa Mobeto; ni mwanamama staa wa muziki, filamu na mitindo nchini Tanzania ambaye sasa ni zamu yake kutesa na ndinga la kifahari aina ya  Range Rover Evoque lenye thamani ya shilingi milioni 150 za Kitanzania.

 

Ikumbukwe kwamba, kabla ya Hamisa, wengine wanaotamba na Range Rover Evoque na kuwakosesha mabinti wa watu usingizi ni pamoja na waigizaji Kajala Masanja (anazo mbili alizonunuliwa na mchumba’ke, Harmonize) na Irene Uwoya (anazo mbili; moja amenunuliwa na mpenzi wake).

Kwa upande wake, muigizaji Wema Sepetu aliwahi kuendesha Range Rover Evoque enzi zake ambapo alisema lilisababisha kuongezeka kwa ‘hips’ zake, lakini sasa ni zamu ya Hamisa.

 

Baada ya kukabidhiwa ndinga hilo, Hamisa amesema; “Yaani kuna wanaume…alafu kuna mwanaume wangu mimi hapa. Thank you baby….I literally wanna cry…Thank you for showing me what true love is…

 

“You have been nothing but the best thing that has ever happened to me…Nakupenda weeeh…Roho yangu weeee…Kwako sijiwezi…Ohh mai laaaaavuuu…”

STORI NA SIFAEL PAUL

AMBER RUTTY AOMBA TENA RADHI HADHARANI – “NIMEOKOKA, NIMETUBU MAKOSA YANGU ” | KATAMBUGA…

Leave A Reply