The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Awageukia Wanaosema Hatoweza Kuongoza Nchi – Video

0


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Watanzania kuwa ataiongoza nchi vizuri na wale ambao wana mashaka kuwa mwanamke anaweza kupata shida kuongoza nchi basi wasubiri kuona utendaji wake.

 

 

Mama Samia amesema hayo leo wakati akihutubia Taifa katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kwenye shughuli ya kitaifa ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliyefariki dunia machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam kwa ugonjwa wa moyo.

 

“Ni siku nyingine ngumu katika historia ya nchi yetu, tarehe 17 ilikuwa ni siku ngumu nilipotakiwa kutangaza kifo cha Rais haikuwa rahisi nilihisi nafanya makosa kumtangaza Rais wangu amefariki, lakini nikaambiwa hakuna wa kutangaza isipokuwa wewe

 

 

“Kifo ni fumbo kubwa, tulizoea kumuona Dkt.Magufuli akiwa kwenye kile kiti nilichokaa Mimi, leo hatupo nae, Juzi ilinipa ugumu kutangaza kifo cha Rais wangu ila nikaambiwa hakuna mwingine wa kutangaza na leo tena nipo hapa huku Hayati Magufuli akiwa kwenye Jeneza.

 

 

“Nilihusudu utendaji wa Hayati Magufuli tangu nikiwa Waziri, nilipenda michango yake Bungeni, alizijua Barabara zote za Nchi hii kwa majina na urefu wake, hakuogopa kutetea kilicho sahihi kwa maslahi ya Taifa, kwake saa 24 hazikumtosha kwenye kazi.

 

 

“Kwa wale ambao wana mashaka kwamba Mwanamke huyu ataweza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nataka niwaambie aliyesimama hapa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye maumbile yake ni mwanamke.

 

 

“Kwa tuliofanya kazi na Hayati Magufuli tunamjua alikuwa ni Mtu anayependa utani, wakati mwingine alitupigia simu Wasaidizi wake na anakuuliza upo na Mumeo hapo mpe simu niongee nae, au Wanaume anawaambia upo na Mkeo hapo naomba niongee nae na hapo utani huwa mwingi.

 

 

“Hayati Magufuli alikuwa Muungwana aliyeona fahari kumsifia Mtu akiwa bado hai, hakuwa Mtu wa kujikweza ndio maana kwenye shughuli zote mliowaona Wastaafu, niwaombe Wastaafu Mimi ni Kijana wenu, hakuna kitakachoharibika, tutaendeleza alipoishia, tutafika alipopatamani,” Mama Samia.

Leave A Reply