The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Aweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Lindi – Video

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo ya Mtaalamu kutoka katika moja ya Vyumba vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mikoa ya Kusini tarehe 19 Septemba, 2023.
Wananchi wa Mkoa wa Lindi wakiwa kwenye Mkutano wa Hadhara wa Rais Samiakatika eneo la Mitwero Mkoani Lindi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mikoa ya Kusini tarehe 19 Septemba, 2023.

Rais Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Lindi, ambayo inatarajia kutoa huduma za afya kwa wagonjwa wa ndani na nje na yenye hadhi sawa na hospitali nyingine kubwa zilizopo nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa pamoja na viongozi wengine wakati akivuta kitambaa kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Lindi katika Kijiji cha Kilangala Mkoani humo tarehe 19 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Lindi iliyopo Kilangala Mkoani humo tarehe 19 Septemba, 2023.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Lindi wakiimba Wimbo Maalum wakati wa mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Shuleni hapo katika Kijiji cha Kilangala hapo Mkoani Lindi tarehe 19 Septemba, 2023.

Leave A Reply