Rais Samia Azindua Minara ya Urushaji wa Matangazo ya Televisheni kwa Kutumia Antena
Rais Samia Suluhu Hassan leo Mei 18, 2023 amezindua minara ya mfumo wa urushaji wa matangazo ya televisheni kwa kutumia antena, yaani mfumo wa Digital Terrestrial Television (DTT).
Minara hiyo iliyojengwa kwenye mikoa 21 na kugharimu jumla ya shilingi bilioni 50 imejengwa katika kipindi cha miaka miwili na miezi sita.
Kwa kuwa na idadi hiyo kubwa ya minara, Azam Media Limited inaongoza kuwa kampuni ya kwanza nchini kwa minara ya Televisheni.
Rais Samia amefanya uzinduzi huo kwenye studio za Azam TV Dar es salaam.
Ahmed Abdalah ambae ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Teknolojia na Miundombinu ndiye mratibu wa mradi huu mkubwa.