The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Azungumza na Mtendaji Mkuu wa Royal Dutch Shell

0

RAIS  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezungumza kwa njia ya Mtandao na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Dutch Shell yenye Makao Makuu yake Nchini Uholanzi Bw. Ben Van Beurden, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 04 Octoba 2021.

 

Ben Van Beurden ameeleza kuwa wanaridhishwa na jinsi Serikali ya Awamu ya Sita ilivyoboresha mazungumzo ya uwekezaji kwenye mradi wa gesi asili iliyosindikwa (LNG) hapa nchini.

 

Kwa upande wake Rais Samia amemshukuru Van Beurden kwa nia yao njema ya kutaka kuwekeza kwenye mradi huo ambao utachochea kukuza uchumi wa Tanzania.

 

Shell yenye makao yake makuu nchini Uholanzi inajihusisha na biashara ya gesi ambapo kwa Tanzania ina ofisi zake kuu jijini Dar es Salaam.

Leave A Reply