The House of Favourite Newspapers

Kocha Simba amvulia kofia Duncan Nyoni

0

KOCHA Msaidizi wa Simba, Seleman Matola, ameonekana kuvutiwa zaidi na kiwango kikubwa kinachoonesha na kiungo wa timu hiyo, Duncan Nyoni raia wa Malawi.

 

Kiungo huyo ambaye ni ingizo jipya ndani ya kikosi hicho, amefanikiwa kucheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara msimu huu na kuuwasha moto unaomfanya Matola kusema: “Huyu ni mtu hatari sana na atakuwa moto wa kuotea mbali siku za mbele.”

 

Matola amesema amekuwa akifuatilia mwenendo wa kiungo huyo anayetumia zaidi mguu wa kushoto na kumuona akibadilika kwa haraka na kuingia kwenye mfumo wa timu hiyo.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Matola alisema kwenye mechi mbili za ligi alizoingia akitokea benchi, kiungo huyo alikuwa akiibadilisha Simba kiuchezaji na kasi ya timu kwenye eneo la ushambuliaji imekuwa ikibadilika pia.

 

“Nyoni ni mtu wa kazi, taratibu sasa ameanza kubadilika na kuingia kwenye mfumo wetu wa uchezaji, naona akienda kuwa msaada mkubwa sana kwenye timu siku siyo nyingi.

 

“Nafikiri hata wewe umeona namna ambayo amekuwa akibadilika na kuongeza kitu kwenye timu yetu pindi anapoingia uwanjani,” alisema Matola.

ISSA LIPONDA, Dodoma

Leave A Reply