The House of Favourite Newspapers

Ambundo Arejea Yanga

0

BAADA ya kupata majeraha ya mkono, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Dickson Ambundo, mapema wiki ijayo anatarajia kuanza mazoezi na kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

 

Ambundo aliumia mkono wakati timu hiyo ikifanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba uliochezwa Septemba 25, mwaka huu.

 

Nyota huyo tangu asajiliwe msimu huu akitokea Dodoma Jiji, hajafanikiwa kucheza mchezo wowote wa Ligi Kuu Bara, huku Yanga wakiwa wamecheza michezo miwili dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ambundo, alisema kuwa: “Kwa sasa ninaendelea vizuri, nimeanza mazoezi ya gym, ila nategemea kuanza mazoezi na timu wiki ijayo.”

LEEN ESSAU, Dar

Leave A Reply