The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Azuru Kaburi la Hayati Dkt. Magufuli

0
Rais Samia Suluhu akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipozuru Kaburi hilo leo Oktoba 14,2021.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi, Oktoba 14, 2021 amezuru na kuweka Shada la Maua kwenye Kaburi la aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais Samia akipokea Gwaride rasmi lililoandaliwa na Vijana wa Chipukizi Tanzania, alipowasili katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita leo Oktoba 14, 2021.

Mhe. Samia amefanya tukio hilo wakati alipofika katika kaburi hilo akiwa njiani akielekea katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita kwa ajili ya hafla ya kuzima Mwenge Maalum wa Uhuru inayofanyika leo uwanjani hapo.

Vijana wa Halaiki

Magufuli alifariki duni Machi 17, 2021 wakati akipatiwa matibabu jijini Dar es Salaam kutokana na maradhi ya moyo yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

Vijana wa Halaiki

 

 

Leave A Reply