The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Kufanya Ziara ya Siku Mbili Burundi

0


Rais Samia Suluhu Hassan, kesho Julai 16, 2021 anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Burundi, kwa mwaliko wa Rais Evariste Ndayishimiye.

 

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu, Rais Samia akiwa nchini Burundi, atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Ndayishimiye kisha atashuhudia utiaji saini wa hati za makubaliano na kuzungumza na waandishi wa habari.

 

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Rais Samia atahudhuria na kuhutubia mkutano wa jukwaa la wafanyabiashara wa Burundi na tanzania kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu fursa za biashara na uwekezaji zilizopo ndani ya nchi hizo mbili.

Leave A Reply